Msanii Willy Paul kutokea nchini kenya amejikuta akiingia kwenye mgogoro na walinzi wa tamasha la Furaha City Festival lililofanyika usiku wa kuamkia leo nchini Kenya baada ya ratiba za kutumbuiza kwenye tamasha hilo kubadilika.
Willy Paul ambae alitakiwa kutumbuiza kwenye jukwaa hilo kabla ya Diamond Platnumz inaelezwa alipokea taarifa ya madiliko ya ratiba kutoka kwa waandaji wa show hiyo huku wakielekeza Diamond ndiyo anatakiwa kuanza kupanda stejini kabla ya Willy Paul kitu ambacho hakukubaliana nacho na kupelekea kuleta mzozo baina ya waandaji hao na walinzi.
Baadhi ya video zinazosambaa mitandaoni zinaonesha Willy akivutana na walinzi na waandaji wa show hiyo kuzuia Diamond asipande kutumbuiza na kutaka ratiba ifatwe kama ilivyopangwa mwanzo. Mashabiki waliohudhulia kwenye tamasha hilo walionekana kutopendezwa na kitendo cha uongozi wa steji kutaka kumpandisha Diamond kabla ya Willy huku wakiimba jina la Pozee.
Baada ya mvutano huo uongozi wa show hiyo uliamua kumpandisha Willy Pozee kama ratiba ya mwanzoni ilivyokuwa ikisema, lakini baada ya show hiyo Pozee alijikuta hawezi kuondoka uwanjani hapo kutokana na magari yake kuzuiliwa kwa maelekezo maalum.
Hata hivyo Diamond Platnumz ilibidi asitumbuize tena kwenye tamasha hilo kutokana na maelekezo aliyopewa na meneja wake Sallam SK.
Leave a Reply