Kwenye mafanikio ya Mbosso, Rich Mavoko kahusika

Kwenye mafanikio ya Mbosso, Rich Mavoko kahusika

Alifanya vizuri tangu alipoibuka Mkubwa na Wanae kupitia Yamoto Band na akaendelea kutamba baada ya kusainiwa na WCB Wasafi, kwa kipindi chote Mbosso amejikusanyia mashabiki kibao kutokana na uandishi wa kipekee alionao na uimbaji wa kuvutia.

Hadi sasa Mbosso aliyesainiwa WCB Wasafi 2018, ameshatoa albamu moja, Definition of Love (2021), Extended Play (EP) moja, Khan (2022) na kushinda tuzo moja ya Muziki Tanzania (TMA) 2022. Fahamu zaidi kuhusu mkali huyo.

1. Jina lake la awali, Maromboso lilikuja baada ya kurekodi wimbo uitwao ‘Maromboso’ kabla ya kulifupisha na kuwa Mbosso baada ya kuchukuliwa na WCB Wasafi mara kundi la Yamoto Band lililoundwa na wasanii wanne, Mboso, Aslay, Enock Bella na Beka Flavour lilipovunjika.

Kwa kiasi fulani hiyo ni sawa na Nay wa Mitego, Mr. Blue na One The Incredible ambao majina yao yanatokana na nyimbo zao za awali kufanya vizuri.

2. Studio ya kwanza kwa Mbosso kurekodi ni Poteza Records chini ya Prodyuza Sule ambaye ndiye alitengeneza nyimbo zilizomtangaza Aslay kama ‘Niwe Nawe’ na ‘Naenda Kusema’ uliobeba jina la albamu yake ya kwanza. 

3. Wimbo wao ‘Yamoto’ ndio wa kwanza kurekodiwa na vifaa vipya vya muziki vya Mkubwa na Wanawe, kufanya vizuri kwa wimbo huu ndio sababu ya kuzaliwa kwa jina la kundi la Yamoto Band.

4. Akiwa na Yamoto Band, Mbosso ndiye alimtambulisha Rayvanny kwa Diamond walipokutana studio kwa Tudd Thomas wakati Chibu anarekodi wimbo wake, I Miss You. Wakati huo Ray ndio alikuwa anatafuta nafasi ya kutoka kimuziki.

5. Baada ya kuvunjika Yamoto Band, Rich Mavoko ndiye alienda nyumbani kwa Mbosso na kumchukua hadi Sinza zilipokuwepo ofisi za WCB Wasafi kwa wakati huo na siku hiyo Mbosso alisaini mkataba wa kuwa chini ya lebo hiyo.

Mbosso alikuwa ameshakata tamaa kuendelea na muziki ila Rich Mavoko alikuwa anamtia moyo kila walipokuwa wanakutana mazoezi ya mpira pande za Tabata.

6. Mbosso ni msanii wa sita kutambulishwa na WCB Wasafi baada ya Harmonize (2015), Rayvanny (2016), Queen Darleen (2016), Rich Mavoko (2016) na Lala Lava (2017). Na baada ya Mbosso (2018), akafuata Zuchu (2020) na D Voice (2023).

7. Akiwa WCB Wasafi tuzo ya kwanza Mbosso kushinda ni kutoka HiPipo Awards 2019 Uganda ambapo video ya wimbo wake, Hodari (2018) ilishinda kama Video Bora ya Mwaka, kisha kushinda TMA 2022 kama Msanii Bora wa Kiume wa Bongofleva.

8. Mbosso ni msanii wa kwanza wa WCB Wasafi kutoa albamu, Definition of Love (2021) na kumshirikisha Diamond kwenye nyimbo mbili (Baikoko na Karibu) kwa wakati mmoja, kisha akafuata D Voice kupitia albamu yake, Swahili Kid (2023).

Rayvanny hakufanya hivyo katika albamu yake, Sound From Africa (2021), Lava Lava katika EP yake, Promise (2021), wala Zuchu katika EP yake, I Am Zuchu (2020).

9. Mbosso ni msanii wa nne Tanzania kufikisha wafuasi (subscribers) zaidi ya milioni 1 YouTube baada ya Diamond, Harmonize na Rayvanny, kisha wakafuata Zuchu, Alikiba, Lava Lava, Nandy, Marioo, Aslay, Rose Muhando, Jux na Jay Melody. 

10. Ikumbukwe Diamond ambaye ameshirikiana na Mbosso katika nyimbo kama Baikoko (2021), Karibu (2021) na Oka (2022), ndiye mwanamuziki anayeongoza Afrika kwa wasuasi wengi YouTube akiwa nao milioni 9.3, huku akiwa wa pili kwa waliotazamwa zaidi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags