Mambo yanayo kwamisha biashara yako isiweze kukua

Mambo yanayo kwamisha biashara yako isiweze kukua

Helooow! Natumai ni wazima wa afya. Leo bwana katika biashara nimekuja na jambo konki yaani ukiweza kulifuatisha hili basi biashara yako haita tetereka, cha kwanza ninacho taka ujue ni kwamba usianzishe biashara kisa rafiki yangu flani ameanzisha no weka mipango na nia haswa kama unataka kuanzisha biashara pia uweke akilini katika biashara hiyo kunachangamoto utakutana nazo

Wafanyabiashara wengi hukumbwa na changamoto nyingi katika uendeshaji wa shughuli zao. Changamoto hizi ndizo zinaweza pia kuwa utofauti wa biashara zinazokua na zile zinazokufa.

VIKWAZO VINAVYO KWAMISHA BIASHARA YAKO ISIWEZE KUKUA 

  1. Kutokuwa na business plan (mpango biashara) 

ni ramani ambayo inaenesha namna unavyotegemea kuendesha biashara na malengo mahususi ya biashara yako.

Business plan ni muhimu kwa mtu anaeanzisha biashara ndogo ili iweza kuwa kubwa na kutambulika zaidi pia hutumika hususani katika makampuni ya wafanya biashara mbali mbali ili kuendeleza biashara yao, watu wengi wananzisha biashara bila kuandika mpangilio wa biashara yake itakavyo kuwa.

2.Ushindani wa kibiashara

Kikwazo hiki kinajitokeza kwa namna nyingi ikiwa ni pamoja na uwezekano mkubwa wa kuigwa na watu wengine, Ni kawaida watu kutaka kuiga kama ufanyavyo hasa pale unapoonekana kufanikiwa. Kikwazo hiki hujitokeza pia katika namna ya bidhaa mpya zinazokuja kuwa mbadala wa bidhaa yako na hata kuwa katika bei ya chini zaidi. 

Kumbuka siku hizi wateja wengi wana mianya mingi ya kupata taarifa za bidhaa mbalimbali na bei zake toka kwa wauzaji mbalimbali Hivyo kufanya biashara kwa mazoea tuu kwakuwa una jina kubwa haitoshi.

3.Mtaji

Kikwazo hiki hujitokeza katika mitazamo mitatu kwanza wakati wa kutaka kuanzisha biashara pili wakati biashara imeshaanza ila fedha hazitoshi kuendesha vema na tatu pale mfanyabiashara anapokusudia kupanua biashara yake. Kwahiyo unapo taka kuongeza mtaji au kuanzisha biashara basi jitasmini na kufikiria kwa undani ili usije kuambulia kupata hasara. 

4.Usimamizi wa wafanyakazi

Mambo magumu yanayojitokeza katika usimamizi wa wafanyakazi ni wafanyakazi kukosa uaminifu na kuwa na ufanisi wa chini ya kiwango. Usipoangalia utapata hasara na hata kupoteza wateja kwani wateja kwa ujumla huja kufuata bidhaa na huduma zako ambazo zinatolewa na hao wafanyakazi. Utakapo wasimamia wafanyakazi wako vizuri basi biashara yako itakuwa kuliko unavyo fikiria mana wafanyakazi ndo chachu ya biashara yako kutambulika zaidi.

5.Ubia

Mara nyingi imekuwa ni ngumu kwa watu wengi kufanya biashara kwa kushirikiana na watu wengine, hususani katika hatua za mwanzo za uanzishwaji wa biashara. Vikwazo vinavyojitokeza katika kufanya ubia na watu wengine ni vingi kama vile, Kutokupata watu waaminifu, Kupata watu wasio na moyo wa kujitolea kufanya shughuli za biashara yenu, kupata watu wanaokuwa wagumu kujitolea mtaji wa kutosha kufanya biashara yenu, na zaidi sana kupata watu wasio na muelekeo au mtazamo wa mbali wa kijasiriamali yaani wao wanawaza faida ya haraka haraka na kwamba kwao biashara ni sehemu ya kuingiza fedha ya ziada tuu ya leo au kesho.

Wanangu wa Mwananchi Scoop ukitaka kuanzisha biashara lazima ufuatilie kwa undani faida na hasara katika biashara unayotaka kuianzisha, location nzuri utakayo fanyia biashara yako iwe ni sehemu ambayo inamzunguko wawatu chingine cha muhimu ni kuweka akiba.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags