Manara Aendelea Na Msimamo Wake

Manara Aendelea Na Msimamo Wake

Aliyekuwa mume wa mwigizaji Zaiylisa, Haji Manara ameendelea na msimamo wake wa kutoongea chochote mpaka pale muda sahihi utakapo amua hilo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram amewataka waandishi wasiendelee kumtafuta kwani hana majibu ya kuwapa kwasasa.

“Waandishi wa habari msihangaike kunitafuta na kunipigia, Jibu langu kwa hili liliotokea ni lile lile moja NO COMMENT kwa sasa !!, Nimeamua kukaa kimya ili muda sahihi uje kuongea
wenyewe.

Nawapenda sana Wanahabari wenzangu, na nnajua mayo haki ya kusikia ya upande wa pili,, lakini kwa heshma kubwa nawaomba mnielewe msimamo wangu
huu, Content hii ubora wake ni ukimya wangu, zaidi ya kile nilichoandika juzi!!
Hope mtanielewa my colleagues,”ameandika Manara.

Utakumbuka kuwa siku moja iliyopita wawili hao waliingia kwenye ugomvi mkubwa uliopelekea Zay kuomba talaka huku wakirushiana maneno katika mitandao ya kijamii.

Wawili hao walifunga ndoa Januari 24,2024, ikiwa ndoa ya sita kwa Manara na ya pili kwa Zaiylissa






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags