Marekani Ilivyomuharibu Mtoto Jackie Chan

Marekani Ilivyomuharibu Mtoto Jackie Chan

Mwigizaji na mtayarishaji wa filamu kutoka Hong Kong, Jackie Chan alifunguka kuwa moja ya sababu iliyomfanya mwanae kuharibika na madawa ya kulevya ni kutokana na mazingira ya Marekani.

Wakati akiwa kwenye moja ya mahojiano yake na gazeti la ‘South China Morning Post’ alidai kuwa mtoto wake Jaycee Chan alikulia katika mazingira ya Marekani ambapo alikosa nidhamu na maadili ya familia, jambo lililochangia katika tabia zisizofaa ambazo amekuwa akizionesha.

“Nilijua kuwa nilikosea kumlea mtoto wangu. Nilimlea kwa namna isiyo bora, nikimuachia aishi Marekani ambapo alijikuta akikosa maadili na nidhamu. Nilitaka kumfundisha umuhimu wa kazi ngumu na nidhamu, lakini nilikosea,”

Chan aliongeza kuwa alijivunia mafanikio yake kama mchezaji filamu, lakini anajiona dhaifu kuwa mzazi ambaye ameshindwa kutimiza majukumu yake ya kumlea mtoto wake katika njia sahihi.

Ikumbukwe Jaycee Chan alikamatwa mwaka 2014 nchini China kwa kumiliki na kutumia dawa za kulevya, ambapo alihukumiwa kifungo cha miezi sita gerezani. Jackie Chan alielezea huzuni yake kuhusu tukio hilo na alikiri kwamba alikosa kumfundisha mtoto wake maadili na nidhamu bora.

Aidha kutokana na suala hilo mwaka uliyoisha 2024 alitangaza nia ya kuchangia utajiri wake wote, unaokadiriwa kufikia dola 400 milioni 'Sh 966 bilioni', kama msaada kwa watu wenye uhitaji huku akiwataka watoto wake kujitengenezea pesa zao wenyewe.

Nyota huyo alipata umaarufu kupitia filamu zake kama Drunken Master (1978), Police Story (1985), Rush Hour (1998), The Karate Kid (2010) na nyinginezo






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags