Mwimbaji wa merengue mwenye umri wa miaka 69 kutoka Jamhuri ya Dominika, Rubby Pérez anayejulikana kwa vibao vilivyotamba kwenye Billboard kama “Tu Vas a Volar,” “Enamorado de Ella” na “15,500 Noches” amefariki dunia pamoja na mashabiki wake baada ya kuangukiwa na paa.
Taarifa ya kifo chake ilithibitishwa na meneja wake, Enrique Paulino jioni ya jana Jumanne Aprili 9,2025 kupitia mitandao ya kijamii ya msanii huyo.
Aidha Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Dominika lilithibitisha kuwa watu 80 wamefariki kutokana na kuporomoka kwa paa hilo hadi Jumanne usiku. Huku mpaka kufikia sasa, jumla ya watu 155 wakifikishwa katika vitoa vya afya kwa ajili ya matibabu.
Ikumbukwe msanii huyo na mashabiki wamefariki wakati wa tamasha lake ambalo lilifanyika katika klabu ya usiku iitwayo ‘Jet Set’ mapema wiki hii.
Miongoni mwa waliothibitishwa kufariki pia ni Tony Blanco, mchezaji wa zamani wa Major League Baseball na baba wa mchezaji chipukizi wa timu ya Pittsburgh Pirates, Tony Blanco Jr, Nelsy Cruz, gavana wa jimbo la Montecristi kaskazini-magharibi mwa Jamhuri ya Dominika na wengineo.

Leave a Reply