
Mwakinyo Ashikiliwa Na Polisi, Sababu Yatajwa
Bondia wa ngumi za kulipwa nchini na bingwa wa mkanda wa WBO Afrika katika uzani wa middle, Hassan Mwakinyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga akituhumiwa kum-shambulia mtu anayedaiwa kuingia katika eneo lake bila ya ridhaa yake.
Mwakinyo anashikiliwa na jeshi hilo tangu jana Alhamisi katika Kituo cha Chumbageni kutoka-na sakata hilo, huku mtu aliyemshambulia akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo Tanga.
Sababu kubwa ya bondia huyo kushikiliwa na jeshi hilo ni kutokana na madai ya kumshambu-lia mtu huyo na kumsababishia majeraha ma-kubwa mwilini.
Mwananchi limemtafuta Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, ACP Maket Msangi am-baye amekiri kuwa wanamshikilia bondia huyo maarufu nchini.
“Tunamshikilia Hassan Mwakinyo, hatumshikilii bondia. Hakuna shida ila ana tuhuma za kum-shambulia mtu ambaye inasemekana alipita maeneo ya nyumbani kwake na kujaribu kuin-gia kwa namna ya mazingira ambayo inadaiwa ni kwa nia ya kutenda kosa, kwa hiyo akamka-mata," amesema Msangi.
“Wakati tunapewa taarifa alikuwa amemkamata, polisi tulienda kwa ajili ya kumchukua mtuhumiwa lakini alikuwa kidogo ana majeraha, tukampeleka akapate huduma ya kwanza Bombo kwa hivyo tunamshikilia kutokana na kumkuta mtuhumiwa kidogo ana majeraha, Tunaendelea kumhoji Mwakinyo kwa nini mpaka akajeruhiwa hivyo."
Leave a Reply