Mwanamuziki Tina Turner afariki dunia

Mwanamuziki Tina Turner afariki dunia

Nyota mkongwe wa Muziki wa Rock 'n' Roll kutoka nchini Uswisi amefariki dunia nyumbani kwake huko Kusnacht akiwa na umri wa miaka 83 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa familia, Turner aliyezaliwa Tennessee, Marekani alianza kuwa na hali mbaya ya Kiafya baada ya kugundulika kuwa na Saratani ya Utumbo mwaka 2016 na kupandikizwa Figo mwaka 2017.

Aidha enzi za uhai wake, alifanikiwa kushawishi wanawake wenye asili ya Afrika kufanya muziki wa Rock 'n' Roll huku akitamba na nyimbo kama 'Whats Love Got To Do With It' na 'Proud Mary'.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags