Ndoa ya Lopez yapumulia mipira

Ndoa ya Lopez yapumulia mipira

Mwigizaji na mwanamuziki wa Marekani, Jennifer Lopez, ameripotiwa kufungua shauri la kudai talaka kwa mumewe, Ben Affleck.

Kwa mujibu wa TMZ, Lopez amewasilisha shauri hilo mahakama kuu ya Los Angeles jana Jumanne Agosti 20, 2024 akiwa mwenyewe bila ya wanasheria wake.

Aidha katika hati hizo zilizofikishwa mahakamani zinaeleza kuwa ndoa ya wawili hao haikuwa na mkataba wa kisheria wa mgawanyo wa mali hivyo huenda mali zote ambazo kila mmoja alizichuma kabla ya ndoa hazitokuwa za pamoja pale ndoa itakapovunjika.

Wawili hao walianza mahusiano baada ya kukutana kwa mara ya kwanza kwenye maandalizi ya Sinema ya Gigli mwaka 2002, walichumbiana mwaka huohuo mwezi Novemba huku wakipanga kuoana Septemba 2003 lakini ndoa iliahirishwa, waliachana 2004 na kurudiana 2021, wakafunga ndoa 2022 lakini walikuja tena kuzinguana Aprili 26, 2024.

Mbali na kuwasilisha talaka hiyo utakumbuka kuwa wiki chache zilizopita Lopez na Affleck walitangaza kuuza nyumba yao iliyopo Beverly Hills ambapo kwa sasa Ben anaishi kwenye nyumba aliyoinunua huko Brentwood huku Lopez akidaiwa kutafuta nyumba mpya.

Hii inakuwa ndoa ya nne ya Lopez kuvunjika kwani aliwahi kufunga ndoa na mastaa kama Ojani Noa (1997), Cris Judd (2001) na Marc Anthony (2004).






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags