Nyota wa Disney Coco Lee afariki dunia

Nyota wa Disney Coco Lee afariki dunia

Mwimbaji Coco Lee, mzaliwa wa Hong Kong aliejizoelea umaarufu katika Pop huko Asia miaka ya 1990 na 2000 amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 48.

Lee alihamia Marekani akiwa mtoto na akatoa albamu katika lugha za Mandarin na Kiingereza. Pia alikuwa mhusika mkuu katika toleo la lugha ya Mandarin katika filamu maarufu ya Disney ya Mulan, na akaimba wimbo kwa sauti ya Crouching Tiger, Hidden Dragon katika Tuzo za Oscar za 2001.

Kupitia taarifa ya dada zake wakubwa Carol na Nancy walioichapisha kwenye mtandao wa facebook “alikuwa akiugua mfadhaiko kwa miaka michache. Alijaribu kujiua akiwa nyumbani Jumapili na akapelekwa hospitalini, ambapo alifariki Jumatano” waliandika

Ikumbukwe tu Lee aliingia katika kitengo cha pop ya lugha ya Mandarin maarufu kama Mandopop mnamo 1994 na kutoa albamu mbili katika lugha ya Mandarin na mwaka uliofuata, alitoa albamu ya lugha ya Kiingereza na albamu ya tatu ya Mandarin.

“Siyo tu kwamba alituletea furaha na nyimbo na dansi zake katika kipindi cha miaka 29, pia alifanya kazi kwa bidii kuwafungulia waimbaji wa Kichina katika anga ya kimataifa ya muziki na amekuwa akifanya kila awezalo kuwaangazia Wachina” dada zake Lee waliandika.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post