Nyuma ya pazia rangi nyekundu ya mdomoni

Nyuma ya pazia rangi nyekundu ya mdomoni

Rangi nyekundu ya mdomoni ‘lipstick’, si mtindo wa kisasa kama ambavyo wengi wanavyofikiria, mtindo huo ulianzishwa na wanawake wa Babeli na Sumeria kutoka Mesopotamia ‘Iraki’ zaidi ya miaka 5,000 iliyopita, ambapo walitumia udongo mwekundu, madini pamoja na mabaki ya wadudu wenye rangi nyekundu kupaka mdomoni.

Aidha urembo huo haukuishia miaka hiyo kwa familia za kifalme bali uliendelea na kuja kupamba moto nchini Misri ambapo Cleopatra alinogesha uzuri wake kwa kupaka rangi nyekundu mdomoni akitumia mchanganyiko wa wadudu aina ya ‘cochineal’ na unga wa lulu ili kuzipa muonekano mzuri lipsi zake.

Wakati wa Warumi, rangi hiyo ilipendwa zaidi na wanawake wa tabaka la juu, waliitengeneza kwa kutumia udongo, mafuta ya mzeituni na nta ya nyuki.

Lakini baada ya kuanguka kwa Dola ya Roma, mambo yalienda kombo ambapo Ulaya ya zama za kati ilihusisha rangi hiyo ya mdomo na uashereti pamoja na ushirikina, huku ikiwatazama wanawake waliopaka rangi hiyo kama wachawi na wenye tabia mbaya.

Kadri siku zilivyozidi kwenda mtazamo huo ulibadilika, karne ya 16 urembo huo ulimpa mwonekano wa kuvutia Malkia Elizabeth I wa Uingereza licha ya kutengenezwa na malighafi zilizo na sumu lakini wanawake wa nchini hawakukoma kuitumia.

Karne ya 19 ilipoanza, mapinduzi ya viwanda yalibadilisha kila kitu. Lipstick ikaanza kutengenezwa kwa teknolojia ya kisasa, mwaka 1884, kampuni ya Guerlain kutoka Paris ilizindua lipstick ya kwanza iliyofungwa vizuri, hatua iliyofungua njia za kibiashara katika mataifa mbalimbali. Kwa sasa rangi nyekundu ya mdomoni ni alama ya urembo na ujasiri duniani kote.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags