Waandaji wa Tuzo za ‘The Academy Awards’ 'Oscars' wamefanya mabadiliko kuelekea msimu ujao wa tuzo hizo. Huku wakianzisha sheria mpya kwa wapigaji kura pamoja na waandaji wa filamu.
Kufuatia na taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo imeelezwa kuwa wapigaji kura wote wanatakiwa kutazama kila filamu iliyoteuliwa katika vipengele mbalimbali kabla ya kupiga kura.
Kwa mujibu wa ‘NBCDFW’, hatua hii imelenga kuboresha uadilifu na usawa katika mchakato wa upigaji kura, kwani baadhi ya wapiga kura wamekiri kupuuza baadhi ya filamu au kupiga kura kwa kuzingatia umaarufu wa msanii na filamu badala ya ubora.
Aidha mbali na sheria mpya ya kutazama filamu kabla ya kupiga kura. Pia waandaji wa tuzo hizo wameweka wazi kuwa filamu zitakazotengenezwa kwa msaada wa akili bandia (AI) zitaweza kushinda tuzo kuu katika Oscars.
Hata hivyo kuwepo kwa kipengele cha Filamu Bora ya Kimataifa, ambapo waandaaji wa Oscar watawaruhusu waandaji wa filamu kutoka nchi nyingine, wakimbizi kuwasilisha filamu zao ambazo pia zitapewa kipaumbele kuwania tuzo hizo.
Tuzo za 98 za Academy Awards (Oscars) zitafanyika Jumapili, Machi 15, 2026 katika ukumbi wa Dolby Theatre, Hollywood, Los Angeles. Huku Mchekeshaji maarufu Conan O’Brien atarejea kama mwenyeji wa hafla hiyo kwa mwaka wa pili mfululizo.

Leave a Reply