R Kelly Azua Vurugu Gerezani, Adai Anaonewa

R Kelly Azua Vurugu Gerezani, Adai Anaonewa

Mwanamuziki wa R&B kutoka Marekani, Robert Sylvester Kelly maarufu R. Kelly, ameripotiwa kuzua vurugu za kupiga kelele na kulia akiwa gereza la Butner Federal Correctional Complex, North Carolina ambapo anatumikia kifungo chake.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa maafisa wa magereza, R. Kelly, ambaye anatumikia kifungo cha miaka 30 kwa makosa ya unyanyasaji wa kingono na utekaji nyara, alianza kupiga kelele usiku wa manane akilalamikia hali ya afya yake na kudai anaonewa.

Aidha mashuhuda wamedai kuwa walinzi wa gereza walilazimika kuingilia kati na kumtuliza ili kuepusha usumbufu kwa wafungwa wengine.

Utakumbuka msanii huyo alipelekwa hospitali ya Duke University Hospital, Durham Juni 13,2025 baada ya kuanguka ghafra huku chanzo kikiwa ni kupewa dawa nyingi gerezani ambapo alitoka hospitali hapo Juni 15 baada ya kupokea matibabu ya siku mbili.

Hata hivyo kwa mujibu wa vyanzo vya karibu vinadai kuwa polisi walimrudisha kwa nguvu gerezani licha ya madaktari kuwaeleza kuwa mgonjwa anahitaji kukaa hospitalini kwa takriban wiki moja ili kuchunguza tatizo jipya la uvimbe wa damu katika mapafu na miguu.

Wakili wake ameiomba mahakama izingatie hali yake na kupunguza adhabu au kumpa dhamana kwa misingi ya afya, lakini ombi hilo bado halijapatiwa uamuzi wa mwisho. R. Kelly amekuwa akikanusha madai yote dhidi yake na anapanga kukata rufaa akiendelea kushikilia hana hatia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags