Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Dk Patrice Motsepe amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha mchezaji wa klabu ya Modern Future ya Misri, Ahmed Refaat.
Kupitia barua aliyokiandikia Chama cha Soka cha Misri (EFA), Dk Motsepe ametuma salamu za rambirambi binafsi na za CAF kwa familia ya nyota huyo wa zamani wa Zamalek, ENPPI, Al Masry, Al Ittihad, Al Wahda na mwisho Future FC pamoja na marafiki, wafanyakazi wenzake na EFA kwa ujumla juu ya msiba huo.
Mchezaji huyo aliyewahi kuichezea timu ya taifa ya Misri, amefariki dunia kutokana na mshtuko wa moyo alioupata tangu Machi 11, 2024.
Refaat alikuwa na matatizo ya kiafya katika wiki za hivi karibuni baada ya kuanguka uwanjani kufuatia shambulio la moyo kwenye mchezo dhidi ya Al Ittihad ya Alexandria uliopigwa Machi kabla ya kuwahishwa hospitalini na kuruhusiwa baada ya kupata fahamu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply