Saluh Wa Bss, Lwaga Wamkosha Bien

Saluh Wa Bss, Lwaga Wamkosha Bien

Mwanamuziki kutoka nchini Kenya, Bien ambaye amewasili Bongo kwa ajili ya kukiwasha katika show ya Darassa ‘Take Away The Pain album Tour’ ameeleza namna ambavyo anakoshwa na vipaji vya Bongo kikiwemo cha mshiriki wa BSS, Saluu.

Wakati akizungumza na waandishi wa habari usiku wa kuamkia leo Aprili 25,2025, Bien amefunguka mengi huku akiwasifia wasanii wa Tanzania katika Live Perfomance akimtaja msanii wa nyimbo za injili, Joel Lwaga na mshiriki wa Bongo Star Search, Saluu kama mfano.

“Mimi nikiangilia Tanzania Live Perfomance naangaliaga wale wasanii wenu wa Gospel, kuna mtu anaitwa Joel Lwaga ni mnyama balaa, Gospel kwa Tanzania hata hatuwagusi tukiimba live waimbaji wa Gospel Tanzania wache.

Halafu kuna Star Search fulani nilionaga Tiktok kuna kijana alikuwa anaimba nyimbo za Diamond anaitwa Saluu, Huyo jamaa ni mnyama Live misijaona mtu kama huyo Afrika Mashariki" amesema Bien.

Aidha msanii huyo alitia neno katika ishu ya Mastar Jay kumtaja kuwa Alikiba hajui kuimba huku akiweka wazi kutopendezwa na kauli alizozitoa.

“Achana na Master Jay achana na hiyo stori, harafu pia Mastaer Jay acha kufanya hayo hayapendezi kabisa mimi binafsi sikupenda alichokizungumza.

Halafu Afrika Mashariki sasa hivi ni muda wa kujenga, miaka mitano ijayo wakina Saluu watakuwa wanatuuliza nyie wazee mlikuwa mnafanya nini hatuwezi kuwaambia tulikuwa na bifu, lazima tufanye muziki kwaiyo Master Jay hicho ulichokifanya sio sawa,” amesema Bien.

Hata hivyo aliongezea kwa kumtaka Master Jay ajiheshimu kwani kwa umri wake hapaswi kufanya mambo kama hayo mitandaoni.

“Kwa heshima yake amefanya vitu vikubwa nimekuwa nikisikiliza muziki wake ametayarisha baadhi ya nyimbo kubwa na Hit za Bongo Fleva kwaiyo ni mzee noma lakin alichokifanya hakiwezi kujenga chochote.

Siwezi mwambia nini afanye, amenizidi umri labda yeye anambie mimi chakufanya, namuheshimu sana lakini nisingependa iende huko kwa sababu hiyo ni sumu,” amesema Bien.

Mbali na hayo alifunguka kuhisiana nayeye kupendelea sana kuja Tanzania mara kwa mara huku akiweka wazi kuwa Wakenya na Watanzania ni Ndugu.

“Mimi ndugu yangu ambae namfuata ameoa Tanzania, ameoa Moshi nimeenda mpaka Moshi nimekunywa Mtori huko, nimekula nyama ya mbuzi laini lakini pia nina stori moja na Ambwene 'AY' lakini hiyo siwezi isema hapa.

Unajua Tanzania minadhani tulidanganywa na Wakoloni, walitucholea mipaka lakini ukiangalia kiuhalisia Watanzania ni kama Wakenya, Chakula cha huku ni kama cha Kenya na kinaweza kuwa ni kitamamu kuliko cha Kenya,”amemalizia Bien.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags