Shamsa Ford: Manara Usichoke Kuoa

Shamsa Ford: Manara Usichoke Kuoa

Mwigizaji na mfanyabiashara Shamsa Ford amemtaka aliyekuwa msemaji wa Yanga, Haji Manara asichoke kuoa kwani amekuwa msaada mkubwa kwa wanawake anaofunga nao ndoa.

Inawezekana una matatizo yako ambayo hatuyajui maana ndoa ina mambo mengi. Lakini mimi naongelea mambo tunayoyaona kwa macho. Una moyo safi wewe si mwanaume mchoyo ndio maana ukiwa na mwanamke unampa THAMANI kubwa mpaka Watu watamjua mwisho wa siku inamsaidia mwanamke kupata kazi nyingi sehemu tofauti.

Kaka yangu usichoke kuoa maana pia zinaa ni dhambi, Ipo siku Mungu atakupa mwanamke wa ndoto żako na mtazikana inshaallah, Hakuna mtu anayependa kuoa na kuacha kila siku ni mitihani tu. Pole Kaka yangu kwa yote,”ameandika Shamsa

Aidha kupitia posti hiyo Manara alijibu kwa kuandika “My Sister,,inshaallah tuombeane mema na kukumbushana Asante sana,”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags