Ni ngumu kutaja orodha ya wasanii wakike wakubwa duniani na kuliacha jina la malkia wa pop Beyonce. Lakini licha ya umaarufu na mafanikio yake nyota huyo amekuwa akikosa amani kutokana na mwonekano wa masikio yake anayodai kuwa ni makubwa.
Wengi wanaweza kudhani ni mtindo wake wa fashion kuweka nywele ndefu zenye kufunika masikio na kuvaa hereni nyingi na kubwa, lakini ukweli ni kwamba nyota huyo hutumia mtindo huo kuficha masikio yake.
Anaamini uchaguzi wa hereni kubwa na nyingi ni njia ya kuwafanya watu wasizingatie masikio yake badala yake washangae muundo wa hereni.
Katika moja ya mahojiano aliyowahi kufanya na ITVX alipoulizwa sehemu zipi za mwili wake anatamani kuziboresha, nyota huyo alitaja miguu na masikio.
"Kama ningeweza kubadilisha sehemu moja, ingekuwa miguu yangu. Baada ya miaka yote ya kucheza, imechoka kidogo. Na ninavaa hereni kubwa kwa sababu sipendi masikio yangu,"alisema Beyonce katika mahojiano yake hayo

Leave a Reply