Simba, Kiba, Konde uso kwa uso kwenye Listening Party Ya Marioo

Simba, Kiba, Konde uso kwa uso kwenye Listening Party Ya Marioo

Wanamuziki maarufu wa Bongo Fleva ambao wanaushindani mkubwa katika tasnia ya muziki Diamond, Alikiba na Harmonize wanatarajiwa kuonana uso kwa uso katika sherehe ya ‘Listening Party’ iliyoandaliwa na msanii Marioo ya kusikiliza album yake ya ‘THE GOD SON’.

Sherehe hiyo ya kusikiliza nyimbo zote zilizopo kwenye album hiyo inatarajiwa kufanyika leo Novemba 28, katika ukumbi wa Tips Cocobeach jijin Dar es Salaam.

Marioo aliachia orodha ya nyimbo zilizomo kwenye album hiyo wiki moja iliyopita huku akiwashirikisha wasanii kutoka nje akiwemo Patoranking, Kenny Sol, Bien na kwa upande wa Bongo akifanya kolabo na Harmonize, Aslay, Alikiba na wengineo.

Mbali na wasanii hao mastaa wengine watakao hudhulia katika Listening Party ya THE GOD SON ni pamoja na Zuchu, Chino Kidd, Stan, Mbosso, Mbuzi, Gigy Money, Nandy na wengineo.

Hii itakuwa album ya pili kwa msanii huyo kwani mwaka 2022 aliachia album aliyoipa jina la ‘The Kid You Know’ ikiwa na nyimbo 21.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags