Siri ya mbegu na ganda la tikiti kwa wapenzi

Siri ya mbegu na ganda la tikiti kwa wapenzi

Tikiti maji ni moja ya mazao ya kifahari duniani. Tunda hili ni chanzo kikuu maji na ni muhimu kwa mwili wa binadamu. Wataalamu wanaelezea tikiti maji kama tunda ambalo ni muhimu sana kwa afya ya binadamu, kwasababu ina madini ya hali ya juu ya ikiwa ni pamoja ya vitamini, midini, vizuia oksidi na mafuta.

Tikiti maji lina asilimia 92 ya maji, ikimaanisha kuwa wale wanaotumia tunda hilo hawana hofu ya kukabiliwa na ukosefu wa maji mwilini, anasema mtaalamu wa masuala ya lishe bora Maijidda Badamasi Burji.

Zifuatazo ni faida tisa za tunda la tikiti maji kwa mwili wa binadamu kwa mujibu wa wataalamu:

  • linaongeza maji mwilini

Maji ya na umuhimu mkubwa kwa mwili wa binadamu, ndio maana watu wanakunywa maji kwa wingi ili kuboresha afya zao.

Wataalamu wanashauri matumizi ya tunda la tikiti maji ambalo lina asilimia 92 ya maji, utafidia haja ya kunywa maji zaidi. Tunda hili pia lina madini ya hali ya juu inayosaidia mwili wa binadamu.

  • Lina vitamini na madini mengine

Tikiti maji ni moja ya matunda na mboga ambazo zina kiwango cha chini cha mafuta. Kiwango cha mafuta katika tunda la tikiti maji kiko chini ikilinganishwa na matunda mengine. Kikombe kimoja cha maji ya tikiti maji kina madini aina ya Vitamini C, A, Potassium, Magnesium, Vitamini B1, B5 na B6.

  • Ni k inga dhidi ya saratani

Miongoni mwa virutubisho vinavyopatikana kwenye tikiti maji ni kinga dhidi ya aina fulani za saratani

Utafiti hata hivyo unaonesha kuwa watu wanaokula tikiti maji wana uweze mkubwa wa kupata tiba ya saratani ya tumbo.

  • Kinga dhidi ya maradhi ya moyo

Wataalam wanasema kwamba ugonjwa wa moyo ndio chanzo kikuu cha vifo ulimwenguni. Hatahivyo, imegundulika kuwa aina fulani za virutubisho hupunguza hatari ya mshtuko wa moyo na kiharusi kwa kupunguza shinikizo la damu na kupunguza mafuta mwilini.

Lishe nyingi kwenye tikiti maji zinaweza kutoa uponyaji na kusaidia katika vita dhidi ya magonjwa haya.

  • Ni ngao na nguvu

Tikiti maji huupa mwili kinga, husaidia virutubisho vinavyosaidia mwili kupambana na magonjwa na kupata kinga kutokana na magonjwa au kuumia, na hutibu uchovu na kudorora. 

  • Husaidia kuimarisha afya ya macho

Kunywa sharubati ya tikiti maji huimarisha afya ya macho na kuyalinda dhidi magonjwa mengine mabaya ambayo huenda yakasababisha upofu.

Watu wanaokunywa juisi ya tikiti maji mara kwa mara au kuweka tone lake kwenye macho wanapokuwa wazee hupata kinga kamili ya mwili kwa mujibu wa wataalamu.

  • Inasaidia kupunguza Kuvimba kwa viungo

Citrulline, inayopatikana kwenye tikiti maji inasaidia kupunguza kuvimba kwa viungo vya mwili. Pia inatumiwa kutengeza dawa za kuzuia kuvimba.Kunywa juisi ya tikiti maji kunamsaidia mtu dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Basir.

  • Hurekebisha ngozi na mwili

Vitamini A na C inayopatikana kwenye tikiti maji ni muhimu sana kwa kutoa collageni ambayo inafanya mwili kuwa laini na wa kupendeza. Pia inarekebisha nywele zilizoharibika.

  • Husaidia kumen'genya chakula

Tikiti maji ina maji mengi hivyo kuitumia kwa wingi kunasaidia kusaga chakula. Kunywa sharubati ya tikiti maji mara kwa mara kunasidia mwili kumeng'enya chakula kwa haraka.

Naona nimewachosha wengi lakini natumai umejifunza jambo hapa kuhusiana na tunda hilo la tikiti, sasa hapa ndo tunakuja pale kwenye ile siri ya tikiti maji kwa wapenzi

Hizi ndo siri za mbegu ya tikiti maji?

Huenda wewe ni mmoja wa wale wanaotupa mbegu za tikiti maji - au kuyatoa kabla ya kutumia. Hivi hapa ni vidokezo ambavyo huenda vikakusaidia kubadili mtazamo wako kuhusu mbegu za tikiti maji kwa mujibu wa mtaalamu wa lishe bora.

Hizi ni baadhi ya manufaa ya mbegu za tikiti maji kwa mwili wa binadamu

  1. Zinaongeza nguvu mwilini
  2. Zinaimarisha tendo la ndoa
  3. Husaidia kutatua tatizo la Hedhi kwa wanawake
  4. Huimarisha afya ya akili
  5. hujenga Uboho
  6. Ni ngao ya mwili
  7. Inatibu aina mbili ya Kisukari
  8. Hukuza nywele iliyokatika kwa wanawake
  9. Hurekebisha ngozi
  10. Afya ya moyo

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags