Tanzania namba 4 uzalishaji filamu afrika

Tanzania namba 4 uzalishaji filamu afrika

Wataalamu wa utafiti, mkakati na data ‘Statista’ wametoa orodha ya nchi zinazozalisha filamu huku nchi ya Tanzania ikishika namba nne kati ya nchi 10 barani Afrika kwa mwaka 2021.

Kupitia tovuti ya ‘Statista’ imeripoti kuwa Tanzania huzalisha filamu 500 kwa mwaka huku ikipiga kibuti mataifa mengine kama Tunisia, Uganda, Zambia, Egypt, Liberia Na mengineyo.

Kupitia orodha hiyo iliyochapishwa Januari mwaka huu Nigeria ndio nchi kinara kwa kuzalisha filamu ambapo ililipotiwa kuzalisha filamu 2,599 kwa mwaka 2020 ukiwa ndio uzalishaji mkubwa wa filamu barani Afrika huku namba mbili ikichukuliwa na Ghana ambayo inazalisha filamu 600 kwa mwaka.



Aidha kwa Kenya tasnia ya filamu imeweza kufikia uzalishaji wa filamu 500 kwa mwaka sawa na makadirio ya Tanzania, kwa wastahi huo Afrika inazalisha filamu 5,500 kwa mwaka kulingana na ripoti ya chanzo hicho ilifanywa kati ya Novemba 2020 na Mei 2021.

Hata hivyo huwenda orodha hiyo ikapanda kwa sasa kwani mataifa mbalimbali likiwemo la Tanzania kwa kipindi cha miaka mitatu limekuwa likiwekeza nguvu zaidi katika kiwanda hicho huku baadhi ya wasanii wakivuka mipaka kwenda kujifunza mambo mbalimbali yahusianayo na tasnia ya filamu.

Orodha ya uzalishaji filamu iliyotolewa na Statista
Nigera- 2,599
Ghana- 600
Kenya-500
Tanzania-500
Uganda- 200
Tunisia- 185
Ethiopia- 140
Zambia- 105
Liberia- 100
Egypt- 60






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags