Rapa The Game ameweka wazi kuwa Kanye West alimpatia zawadi ya gari zake mbili aina ya Mercedes-Maybach S680s za mwaka 2025.
Game ameweka wazi kupitia ukurasa wake wa instagram kupokea Gari hizo ambazo alionekana akiendesha kwenye sherehe za ugawaji wa tuzo za Grammys mapema wiki iliyopita.Game ameweka wazi kupitia ukurasa wake wa instagram siku ya ijumaa Februari 7, 2025.
"Ye alinipa maybach mbili siku ya Ijumaa na aliniambia niwaambie “THE DOCUMENTARY 3” itakuwa ya kipekee,”amesema The Game.
TheGame pia alidai Ye alimwagiza auambie ulimwengu kwamba albamu yake ijayo ya The Documentary 3 ambayo Ye ni mtayarishaji mkuu itakuwa ya moto sana japo Albamu hiyo ilidhihakiwa kwa mara ya kwanza mnamo Agosti 2024 wakati The Game alipotangaza kwenye moja ya mahojiano yake.
Ushirikiano huo unakuja baada ya ngoma yao ya Eazy iliyotoka Januari 15, mwaka 2022.

Leave a Reply