Maeneo mengi kwa sasa yanakubwa na mvua. Hivyo ukiwa mdau wa fasheni siyo vizuri kutoka kishamba hata kama mvua inanyesha. Zingatia mitindo hii katika msimu huu wa mvua.
Koti la mvua(Rain Coat)
Kuna aina nyingi za makoti ya mvua ambayo hutengenezwa kwa vifaa visivyopitisha maji. Chagua raincoat lenye rangi nzuri na ya kisasa ili kupata mwonekano bomba na wa kupendeza.
Buti za mvua (rain boots)
Ikiwa maeneo uliyopo yanamadimbwi hakikisha haukozi buti hizo.Kwani zitakupa mwonekano bomba lakini pia zitakufanya kuwa mkavu kwenye miguu yako na hivyo kukuepusha na magonjwa kama fangasi. Katika uchaguzi wako pia zingatia rangi ambayo haishiki uchafu kirahisi ili mwonekano wako usiharibiwe na tope
Shati bomba kwa ajili ya mvua
Katika msimu huu siyo kila aina ya shati unaweza kuvaa ni vizuri kama utavaa yale yaliyotengenezwa kwa pamba. Hii itakusaidia katika kutunza joto ndani.
Mwamvuli wa kisasa
Hakikisha unachagua mwamvuli wa kisasa na unaovutia kwa ajili ya kukufanya uonekane classic. Katika ubebaji wa mwamvuli huo zingatia rangi yake na mavazi utayokuwa umevalia.
Jeans au Suruali taiti
Haipendezi kuvaa sketi au gauni refu katika msimu huu badala yake unaweza kuchagua jeans ambazo zinakauka haraka na zenye ubora wa juu. Pia, unaweza kuchagua 'waterproof trousers' suruali hizi ni nyepesi, rahisi kuvaa, na zina zuia maji.
Gloves
Kama mvua imekuja na baridi, unaweza kuongeza gloves au scarf ili kuongeza joto. Gloves hizi hazipaswi tu kuwa za mvua, bali ziwe katika mtindo wa kuvutia.
Leave a Reply