Watoto Wa Beyonce Na Zigo La Umaarufu

Watoto Wa Beyonce Na Zigo La Umaarufu

Mama mzazi wa mwanamuziki Beyoncé, Tina Knowles ameeleza jinsi alivyo na wasiwasi juu ya changamoto ambazo wajukuu wake wanakumbana nazo kutokana na umaarufu wa familia yao.

Akizungumza na ‘BBC News’ amesema anatamani watoto hao awatenganishe na umaarufu kwani inamtia wasiwasi.

“Kama ningekuwa na uwezo wa kuchagua, ningependa wasikabiliane na mambo wanayokutana nayo kama watoto. Siku moja watasoma ujinga na uongo watu wanaoandika kuhusu wao, na hilo linanitia wasiwasi sana,” amesema.

Hata hivyo, licha ya changamoto za kukua mbele ya macho ya vyombo vya habari na umaarufu. Bibi huyo alimsifu binti yake Beyoncé na mkwe wake Jay-Z kwa jinsi wanavyowalea watoto wao kwa upendo na kujitolea.

“Wanatumia muda mwingi sana na watoto wao, na wana uhusiano mzuri nao. Ni wazazi wa kipekee. Sidhani kama unaweza kutamani wazazi bora zaidi ya hao,” amesema Tina.

Aidha Tina aligusia namna alivyopitia unyanyasaji na familia yake, ikiwa ni pamoja na ubaguzi wa rangi kutoka kwa polisi.

“Kulikuwa na mvutano mwingi wa ubaguzi wa rangi nadhani baadhi ya mambo yamebadilika, lakini bado nadhani watu weusi wanahusika zaidi na ukatili wa polisi," amesema Tina.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags