Ushauri Wa Nenga Kwa Chipukizi

Ushauri Wa Nenga Kwa Chipukizi

Msanii wa Bongo Fleva, Billnass ametoa ushauri kwa vijana na marafiki zake ambao wanavipaji vinavyohusisha umaarufu lakini bado wanajitafuta huku akiwataka kuwa wastamilivu na wavumilivu kwani tasnia nyingi zimejaa mambo mengi mabaya.

“To all Young People, Wadogo zangu na rafiki zangu miliobarikiwa vipaji mbalimbali, Kabla ya kuingia kwenye tasnia yoyote inayohusiana na umaarufu Tanzania!! Muombe sana Mungu akupe nguvu ya uvumilivu na Roho ya kustahimili!! huku kuna kila aina ya vita, Usaliti, Ushetani, Dhuruma kuanzia kwa wadau, Managers, Distribution Company, Labels n.k,” ameandika.



Aidha ameendelea kwa kueleza “Swala la kutajilika au kupata pesa kupitia hizi kazi sio rahisi kama unavosikia ila kupata msongo wa mawazo, kupoteza maisha, kupata maradhi, kuchanganyikiwa ama kuingia kwenye Addiction mbalimbali ni rahisi kuliko kutengeneza pesa, ni vyema kuwa na umakini sana na kuingia kwenye tasnia ukiwa na utayari lakini usiache kumuweka Mungu kwanza.

Maana unaweza kupambana ili uisaidie familia yako kumbe unaenda kuleta janga ambalo familia yako ndo itakuwa kwenye jukumu la kuteseka kukusaidia" Ameandika.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags