Moni: Hakuna Kipengele Kufanya Kazi Na Country Boy

Moni: Hakuna Kipengele Kufanya Kazi Na Country Boy

Msanii wa Hip-hop nchini, Moni Centrozone amewekawazi sababu inayopelekea kundi lao la MOCO lisiwe na mfululizo mzuri wa kuachia nyimbo.

Hii ni kufuatia kutokuwepo kwa mfululizo mzuri wa kuachia nyimbo baina ya wanamuziki hao ambao kila mmoja anafanya kazi kivyake lakini wanapokutana huunda kitu kinachoitwa MOCO wakichukua herufi mbili za mwanzo kwenye majina yao Moni Centrozone na Country Boy.

Akizungumza na Mwananchi, Moni maarufu kama Malume amesema amesema MOCO ilizaliwa baada ya wawili hao kuwa na urafiki, lakini awali kila mmoja alikuwa anafanya kazi kivyake.

“Moco ni kitu ambacho kilizaliwa kutokana na urafiki wetu mimi na Country Boy, na wimbo wetu wa kwanza wa Nikiss Nichum ilikuwa ni wimbo mkubwa kwahiyo ilikuwa na mafanikio makubwa, wimbo huo ulijitokeza wakati Country anatoa kazi zake na mimi natoa kazi zangu, bado hatujasimama vizuri kwahiyo ilikuwa ni swala la muda kutengeneza Legacy ya mmoja mmoja,” amesema Moni.

Ameeleza kuwa licha ya kuonekana nyimbo zao nyingi zinapikwa na mtayarishaji maarufu nchini S2kizzy ‘Zombie’ haimaanishi hawafanyi kazi na watayarishaji wengine.

“Sisi tunafanya na watayarishaji tofauti tofauti mfano Paul Maker, Ammy Wave ni wanetu ambao tumeanzanao kwahiyo hao ni baadhi ya watu ambao tunafanyanao kazi, lakini Zombie ni mtu ambaye tumeshafanyanae sana kazi tangu anaanza kwahiyo muunganiko wetu na S2kizzy ni mzuri kwasababu tulianzanae na tunafahamiana kitambo, japokuwa kuna watu wengine pia huwa wanashiriki, lakini sasahivi tumetengeneza albamu inanyimbo karibia 12 ambazo zote ametengeza S2kizzy" amesema Moni.

Ameongezea kuwa haoni changamoto ya kufanya kazi na Country Wizzy zaidi ni furaha kwa sababu wao ni marafiki nawanafanya kazi kama timu.

“Siwezi kusema hakuna changamoto yoyote, kwanza kazi inakuwa 50 kwa 50 alafu tunakutana katikati, yeye anatoa verse moja mimi moja wimbo unakamilika, wazo la wimbo (Idea), mimi na Country tunaelewana hatujawahi kupishana kauli wala hisia, kwasababu tunaheshimiana sana toka miaka ya nyuma ni watu ambao tunafuraha muda wote utani muda wote,” amesema Moni.

Aidha, amefichua kuwa MOCO ipo mbioni kuachia albamu yenye nyimbo zaidi ya 12 ambazo zote zimetayarishwa na S2kizzy.

“Kama nilivyo sema tumeshatengeneza albamu na S2kizzy kwahiyo mambo mazuri yanakuja kolabo za Kimataifa zakutosha, Sound ya kitofauti kama ulivyoona ‘Pele Maradona’ Billnass yupo ndani lakini pia baadae itatoka ‘Pele Maradona’ Remix kwahiyo kutakuwa na vitu vingi humo ndani,”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags