Wimbo Wa Kendrick Lamar, Beyonce Kutumika Kuokoa Maisha

Wimbo Wa Kendrick Lamar, Beyonce Kutumika Kuokoa Maisha

Shirika la kupambana na matatizo ya Moyo Marekani (AHA) limetumia nyimbo za wasanii kama Kendrick Lamar na Beyonce ili kuhamasisha umma mbinu za kuokoa maisha ya watu kupitia huduma ya kwanza.



Hatua hii inakuja baada ya wawili hao kuondoka na tuzo za kutosha za Grammy 2025. Kupitia ukurasa wa Instagram wa (AHA) umempongeza DJ Mustard ambaye ni mtayarishaji wa “Not Like Us,” huku ukieleza jinsi wimbo huo unaweza kusaidia katika huduma ya kwanza ambapo wamewahimiza watu wanaposhuhudia mtu kaanguka ghafla anapaswa kupiga 911 na kisha kusukuma kifua cha muhusika kwa nguvu na kasi kama midundo ya wimbo huo.



Mbali na huyo pia walimpongeza Beyonce kushinda tuzo ya Grammy kupitia wimbo wake wa “Texas Hold ‘Em” huku wakiwaelekeza watu kutumia sauti ya wimbo huo kama mwongozo kusaidia mtu aliye katika dharura ya moyo.

Aidha ubunifu huo katika kuelimisha umma unakuja wakati magonjwa ya moyo yakiendelea kuwa tishio kubwa kwa maisha ya Wamarekani yamekuwa yakichangia vifo vingi kwa watu wanzima nchini humo huku.

Kwa mujibu wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC), asilimia 22 ya vifo vinavyotokana na magonjwa ya moyo, kiharusi, shinikizo la damu, na mshtuko wa moyo huwapata watu weusi.

Shirika hilo limefanya kampeni hiyo kuwa ya kuvutia na yenye ushawishi mkubwa. Hatua hii inalenga sio tu kuongeza uelewa kuhusu magonjwa ya moyo bali pia kuwahamasisha watu kushiriki katika juhudi za kuokoa maisha kwa mbinu rahisi na zinazoweza kufikiwa na wengi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags