Mwigizaji na mfanyabiashara Jacqueline Wolper ametia neno kuhusiana na ishu nzima ya Zaiylissa na Haji Manara kurushiana maneno mitandaoni huku akiwataka kuacha kutoleana siri.
“Mimi ninachoweza kushauri ni kwamba wapenzi au wanandoa wakigombana wajishikirie zile siri zao wasizimwage hadharani kwa sababu hasira ni kitu kibaya sana na usipo hold hasira yako inaweza ikakufanya ukajijengea uadui mkubwa wa maisha.
Na mimi naamini kugombana au kuacha sio uadui ukiangalia tatizo la kaka na bibie wamefanya vitu yaani wameyatoa ya moyoni, dada alikuwa anakabwa na kaka naye alikuwa anakabwa wakajikuta yai limepasuka. Na ninafikiri katika ile kupasuka kaka atakuwa anajutia kupasuka lakini wifi hajutii ndio kwanza kaita press,”amesema Wolper
Mbali na hilo Mama P alimtaka Zai kutoongea chochote kuhusu Manara huku akitaka amstiri licha ya kuwa na madhaifu.
Mimi nina msihi mdogo wangu Zai hata kama atachokonolewa vipi na waandishi asimseme yule baba vibaya, kwa sababu Zai tulikuwa tunamuona Jua Kali, lakini yale makali aliyoko nayo lakini tumeyaona kupitia kaka kuna mabaya ya mtu lakini kunamazuri yakiwa mengi mstiri kwahiyo nitamuomba sana mdogo wangu Zai amstiri kaka siko upande wowote,”amemalizia Mama P
Hata hivyo alifafanua kuhusiana na sakata lake la kutangaza kuachana na mume wake Rich ambapo alieleza kuwa yeye na mume wake huyo waligombana muda mrefu kabla ya kuweka wazi mitandaoni lakini hakuamua kusema popote kulinda heshima pamoja na biashara zao.

Leave a Reply