Ni ukweli usiopingika Yammi ambaye ni first born wa lebo ya The African Princess ya kwake Nandy ni mmoja kati ya wasanii wa kike Bongo wanaofanya vizuri tangu alipotambulishwa Januari 20, 2023.
KWANINI YAMMI BIDHAA BORA SOKONI
Muziki wa sasa hauhitaji msanii ujue tu kuimba, kuna vitu vya ziada ambavyo inabidi uwenavyo ili kusaidia kusukuma muziki wake kwenda mbele zaidi. Yammi amefanikiwa kuwa na vitu vya ziada ambavyo vinasukuma muziki wake kwa urahisi na kujizolea mashabiki kwa muda mfupi.
Aina ya muziki anaofanya amemua kubaki kwenye Bongo Fleva ambayo imechanganyika na Baibuda tofauti na wasanii wengi wa kizazi hiki kitu ambacho kinampa nafasi ya kuonesha ufundi wake kwenye kuimba zaidi, na watu kukubali uwezo wake wa kufanya muziki.
Yammi tangu ameingia kwenye lebo hiyo ngoma ambazo amekuwa akitoa kama Tiririka zimekuwa na matokeo makubwa kwa sababu ya utofauti wake ambao amekuwa akiufanya kwenye muziki.
Machaguo sahihi ya wasanii wa kushirikiana nao, Yammi amekuwa na collabo ambazo zimepokelewa vizuri kwa mashabiki kutokana na aina ya wasanii ambao amekuwa akishirikiana nao kwenye kazi hizo.
Mei 8, 2024 Barnaba Classic alishirikiana nae kwenye ngoma ya Nibusu, moja kati ya kazi nzuri iliyotoka mwaka huu. Barnaba ni mkongwe kwenye gemu lakini Yammi ndiyo kwanza ana mwaka mmoja na miezi 5 tangu aanze muziki rasmi .
Lakini katika kazi hiyo alionesha ukubwa kitu ambacho kilipelekea kupata remix ya wimbo huo kutoka kwa Mbosso ambaye aliongeza Verse kitu ambacho kiliendelea kuipandisha ngoma hiyo.
Desemba 15, 2023 Yammi alishirikishwa na Abdul Kiba kutoka Kings Music kwenye ngoma ya You, moja katika ya wimbo pendwa kwa mashabiki, huku wengi wakipongeza melodi na mtindo wa sauti anaotumia Yammi .
Piw Septemba 20, Yammi alimshirikisha Mbosso kwenye wimbo wa Nitadumu Nae ngoma ambayo ukiachilia mbali ukali wake wa mashairi uliteka hisia za mashabiki wengi huku wakitamani kuwaona wiwili hao wakiwa Penzini
Kitu ambacho kiliongeza ufuatiliwaji kwa wasanii hao na kuendelea kufanya vizuri zaidi kwenye kazi zao. Ngoma hiyo imekuwa na matokeo mazuri sana mpaka kufikia kutazamwa zaidi ya mara milioni 3 kwenye mtandao wa YouTube.
Licha ya Yammi kuonekana bado kinda lakini tayari ametengeneza ngoma kubwa kama Tiririka ambayo ilitoka Januari 27, 2023 ikiwa imetazamwa zaidi ya mara milioni 12 kwenye mtandao wa YouTube.
Leave a Reply