Zero Brainer Atajwa Tiktok Bora Africa

Zero Brainer Atajwa Tiktok Bora Africa

Mtengeneza maudhui kutoka Tanzania Fanuel John Masamaki, maarufu kama Zerobrainer0, ametajwa kuwa mtengeneza maudhui wa TikTok bora na wakuangaliwa zaidi kwa mwaka 2025 Africa.

Kwa mujibu wa tovuti ya TikTok imeorodhesha watengeneza maudhui sita kutoka Afrika ambao wamekuwa wakifanya vizuri na wakuangaliwa zaidi kwa mwaka huu kutokana na uvumbuzi wanaoufanya katika kutengeneza maudhui yao.

Akiwa na wafuasi milioni 12 ameendelea kutambulika kufuatia na mtindo wake wa kipekee wa maudhui ambao umechanganyika na ucheshi na soka.

Katika orodha hiyo, Kenya pia inawakilishwa na Roy Kanyi, mtaalamu wa teknolojia, huku Nigeria ikiwasilishwa na Tosin Samuel (Tspicekitchen), anayevutia wafuasi katika mapishi, Wengine ni Charity Ekezie kutoka Nigeria, anayepinga dhana potofu kuhusu Afrika kwa kutumia vichekesho na elimu, pamoja na TitoM na Yuppe wa Afrika Kusini, wanaoongoza mitindo mipya ya kidijitali.

Orodha hiyo ya ‘TikTok Discover List 2025’ inawatambua watengeneza maudhui 50 duniani kote, likionesha kuwa jukwa hilo linaendelea kuwa daraja la kuzalisha vipaji na kuwapa hadhi watengeneza maudhui.

Mbali na hilo utakumbuka kuwa mtengeneza maudhui huyo kutoka Bongo siku chache zilizopita alishinda tuzo ya Sports Creator of the Year TikTok Awards 2024 zilizofanyika Johannesburg South Afrika huku ikiwa ni mara ya kwanza kwa Mtanzania kushinda tuzo hiyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags