Oktoba 4, 2006, Jay na mkewe walitembelea eneo la Mwananyamala jijini Dar es salaam ili kuzindua mradi wao wa maji uitwao ‘Water for Life’ lengo kuu la ziara hiyo likiwa ni kuhamasisha na kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo yenye uhaba wa rasilimali hiyo.
Jay akiwa na mke wake walifanikiwa kutengeneza pampu ambayo ilikuwa ikitoa maji safi huku msanii huyo akishirikiana na Umoja wa Mataifa na MTV katika mradi huo.
Hata hivyo ziara hii ilikuwa sehemu ya maandalizi ya filamu ya maandishi ya MTV iitwayo ‘Diary of Jay-Z: Water for Life’ ambayo ilionyesha changamoto za upatikanaji wa maji safi katika nchi zinazoendelea.
Aidha kwenye moja ya mahojiano yake Jay-Z alieleza kuwa alitamani kuisaidia jamii kwa aina yake hivyo akagundua kuwa kunaukosefu mkubwa wa maji duniani ndipo akaamua kujikita katika mradi huo kwa lengo la kupunguza tatizo hilo.

"Nilikuwa natafuta sababu ya kujihusisha nayo. Nilipoona tatizo la maji, na nikaona takwimu zinazohusiana nalo, nilijua hili ndilo nitakalo shughulika nalo,"
Nchi nyingine ambazo wawili hao walitembelea kwa ajili ya kutoa msaada wa maji safi ni pamoja na Kenya, Uganda, Puerto Rico, Nigeria na kwengineko.

Leave a Reply