Basilla Asimulia Alivyokabidhiwa Kijiti Cha Miss Tanzania Na Lundenga

Basilla Asimulia Alivyokabidhiwa Kijiti Cha Miss Tanzania Na Lundenga


Mkurugenzi wa Kampuni ya Look inayoendesha mashindano ya kumsaka Miss Tanzania, Basilla Mwanukuzi ameelezea namna marehemu Hashimu Lundenga alivyomuachia kijiti cha kuongoza mashindano hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 21, 25 baada ya kuaga mwili wa Lundenga nyumbani kwake Bunju B, Ballisa amesema Lundenga alimuuzia leseni za mashindano ya Miss Tanzania tangu mwaka 2018.

"Kwa kweli tumepata msiba mkubwa niseme tumepoteza nguzo ya tasnia ya urembo. Anko Hashim ni mlezi na muasisi wetu mimi mwenyewe ni Miss Tanzania mwaka 1998 ambaye nimetokana na malezi yake.

“Kwahiyo nilipitia jukwaa hili hadi mimi kutambulika katika jamii. Lakini kama mnavyofahamu mashindano ya Miss Tanzania yanamilikiwa na watu binafsi na ni biashara kwa hiyo anko Hashim alivyoona amechoka akaniachia,”amesema Ballisa

Amesema kutokana na yeye kuwa Miss Tanzania 1994 Hashim aliona vyema kumkabidhi kijiti hicho kwani haitakiwa tu biashara badala yake anafahamu nini maana ua Miss Tanzania.

Amesema Lundenga amefanya kazi kubwa kuipambania tasnia ya urembo Tanzania hadi kutambulika katika ngazi ya mashindano ya dunia 'Miss World'.

"Tasnia ya urimbwende inabadilika kipindi chake. Yeye alikuwa na kazi kubwa ya kuitambulisha sanaa hii ili ieleweka kwa watu waelewe sanaa ni nini, urembo ni nini. Mashindano ni nini lakini pia nyakati zake alipigania isiishie tu Tanzania iende katika kinyang'anyiro cha kimataifa kwenye mashindano ya Miss World.

“Kwahiyo alikuwa na kazi ya kutambulisha sanaa kuweka misingi kutengeneza sheria kanuni. Lakini pia mpaka serikali yenyewe kuikubali sanaa. Walikuwa hawaelewi wanasema haya mashindano ni kinyume na mila zetu wakapiga marufuku,”amesema

Amesema kwa juhudi Hashim serikali ikaipokea Miss Tanzania kwa mikono miwili. Kupitia Basata wakatengeneza kanuni ambazo zimeendelea kuboreshwa ili mashindano yawe bora zaidi.

Ameongezea licha ya kuwa nyakati zimebadilika na matamasha yameongezeka lakini bado jukwaa la Miss Tanzania ni ndoto ya wasichana wengi nchini.

"Nyakati zimebadilika zamani tamasha la Miss Tanzania lilikuwa pengine ndio pekee watu wanajua. Siku hizi kuna mambo mengi kuna matamasha ya muziki, watu wana machaguo mengi lakini bado jukwa la Miss Tanzania limeendelea kuwa ndoto kwa binti wa kike,” amesema

Aidha, amesemema mwaka huu 2025 inaandaliwa fainali ya Miss Tanzania baada ya kutofanyika mwaka 2024 kutokana na majukumu yake ya kiserikali.

" Kama mnafahamu mwaka jana mashindano yalifanyika ngazi ya awali tumeona sasa tuandae fainali ambayo haikuandaliwa kama mnavyofahamu mimi nilikuwa kwenye majukumu ya kiserikali. Niliteuliwa na Rais kuwa mkuu wa Wilaya ya Korogwe kwa hiyo nilikuwa nimeachia watu wasimamie.

“Lakini safari hii nipo kwa hiyo tunaandaa tamasha kubwa, shindano ambalo litafanyika Agosti. Kwa hiyo tutampata Miss Tanzania 2025" amesema Basila.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags