Baada ya kuwepo na tetesi kuhusiana na hali ya ndoa ya Justin Bieber na Hailey Bieber kuwa haiko vizuri huku baadhi ya ripoti zikidai kuwa Hailey amekuwa akilia na kuonyesha hofu juu ya mienendo ya Justin, na sasa msanii huyo amekanusha madai hayo akidai kuwa yupo sawa na mke wake.
Kupitia mitandao yake ya kijamii Bieber amefunguka kuhusiana na ndoa yake ambapo ameeleza kuwa kwasasa maisha yake ya ndoa yako imara huku akiwataka watu kuacha kabisa kusikiliza watu wa udaku.
“Mimi na Hailey tupo sawa kabisa. Watu wanaeneza maneno yasiyo na msingi kwa sababu ya wivu lakini ukweli ni kwamba ndoa yetu iko imara, na hatuyumbi. Mimi na Hailey tupo poa kabisa… kelele za mitandaoni hazituyumbishi,”amesema Bieber
Inaelezwa kuwa tetesi hizo za kuwa wanandoa hao kutokuwa sawa ni baada ya Bieber kuonekana akiwa mwenyewe kwenye matembezi pamoja na kuhudhuria kwenye Party bila Hailey huku akionekana anajirusha na rapa Sexyy Red.
Wawili hao walifunga ndoa ya siri mwaka 2018 huku mwishoni mwa mwaka 2024 wakijaaliwa kupata mtoto wao wa kwanza aitwaye Jack Blues Bieber.

Leave a Reply