Polisi Yathibitisha Kumuhoji Mwijaku

Polisi Yathibitisha Kumuhoji Mwijaku

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limethibitisha kuwahoji Mwemba Burton Mwemba, maarufu Mwijaku na wanafunzi wanne wanaidaiwa kushiriki katika tukio la kumshambulia na kumdhalilisha Magnificat Barnabas Kimario ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi. 

Katika taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Aprili 24, 2025, polisi wameeleza kuwa hadi sasa watu wanne wamekamatwa na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo ambalo limelaaniwa vikali na jamii.

“Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Maofisa wa Maendeleo ya Jamii, Idara ya Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, linaendelea na uchunguzi wa tukio la kushambuliwa na kudhalilishwa kwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Magnificat Barnabas Kimario,” imeeleza taarifa hiyo. 

Kwa mujibu wa jeshi hilo, watuhumiwa hao ni Mary Gervas Matogoro, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ryner Ponci Mkwawili, mwanafunzi wa Chuo cha Ardhi, Dar es Salaam, Asha Suleiman Juma, mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu, Dar es Salaam na Mwemba Burton Mwemba, maarufu Mwijaku , mkazi wa Dar es Salaam.

“Upelelezi wa shauri hili upo katika hatua za mwisho na utakapokamilika hatua zaidi za kisheria zitafuatwa dhidi ya wote waliohusika,” imeeleza taarifa hiyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags