Baada ya kuibuka kwa video zikimuonesha baba wa staa wa muziki kutokea Nigeria Asake, akidai hapati huduma kutoka kwa mwanaye. Hatimaye baba huyo amesema tayari ameanza kupatiwa huduma.
Kupitia mahojiano aliyofanya hivi karibuni mzee huyo anayefahamika kwa jina la Fatai Odunsi amesema wamemaliza tofauti na mtoto wake na tayari ameanza kutafutiwa nyumba kwa ajili ya kuishi.
“Asake ameanza kutimiza majukumu yake kwangu kama mtoto wangu. Asake ameagiza watu wanitafutie nyumba ya kununua kwa ajili yangu iliyo karibu na kisiwa (Island). Na kwa saa 24 zilizopita tayari wamekuwa wakitafuta nyumba Hiyo.
"Tumemaliza tofauti zetu, hakuna tatizo tena kati yetu. Pia atahakikisha anamtunza mtoto wake (Zeenat) kikamilifu, pamoja na kugharamia bili zangu za hospitali,"alisema mzee huyo na kuongezea
"Tatizo pekee nililokuwa nalo na mwanangu ni kwamba hakuwa akiongea na mimi kwa muda mrefu. Au hata kujali kuhusu mimi. Kinachoniumiza ni kwamba mama yake hajawahi kumsukuma Asake kuulizia kuhusu hali yangu au kushughulikia mahitaji yangu,” alisema baba wa nyota huyo
Mzee huyo alitawala mitandao ya kijamii nchini Nigeria mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya video yake ikimuonesha anaugulia huku akidai amekosa malezi na msaada kutoka kwa mwanaye staa wa muziki nchini Nigeria, Asake.

Leave a Reply