Aunty Akiri kuzeeka ila Ya Kusah Yanamuumiza

Aunty Akiri kuzeeka ila Ya Kusah Yanamuumiza

Mastaa wengi wa kike baada ya kuanza majukumu ya kulea watoto, bado huendekeza ustaa na kusahau wamekuwa wamama. Wengine hudiriki kutengeneza tena shepu zao ili warudie mwonekana wa awali kabla ha-wajazaa, lakini kwa Aunty Ezekiel kasema usista duu kwake 'No'.

Aunty ambaye ni mwigizaji wa Bongo Movie, hivi karibuni alipata mtoto wa tatu, alisema hana tena muda na mambo hayo na atalea na kuwanyonyesha watoto wake hadi umri unaostahili kama walivyokuwa wakifanya wamama wa zamani.

“Kamwe sitaweka usistaa duu kwenye malezi, tangu nimeanza kupata mtoto wangu wa kwanza hadi huyo wa sasa hivi, sitaweza kwa kweli, kwa sababu nitakuwa siyo mama halisi. Nataka nilee kizamani kabisa kama wazazi wetu walivyotulea na nitanyonyesha hadi mwisho.”

Aunty pia amezungumzia anavyokerwa na kuumizwa na maneno ya watu wanaouandama uhusiano wake na mzazi mwenzake, Kusah kuhusu kumzidi umri kitu ambacho kwake hakimsumbui.

“Kwani wakati tunatongozana hatukujua tunazidiana umri? Mbona watu wanashindwa kufanya mambo ya msingi na kukalia majungu?” aliuliza Aunty.

Ameahidi kulinda uhusiano wake na Kusah ambaye ni msanii wa Bongo Fleva licha ya kuandamwa na maneno.

“Kwetu sisi suala la umri ni namba tu, labda nikuulize, ulishaona mtoto anambebesha mwanamke mimba? Maneno ya mimi kumzidi umri Kusah yananiumiza sana kwa kweli, lakini nitaulinda uhusiano huu hadi mwisho,” alisema Aunt.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags