Beiber ageuka gumzo, ampinguza mkewe

Beiber ageuka gumzo, ampinguza mkewe

Mwanamuziki Justin Bieber amewashtua mashabiki baada ya kufuta urafiki na mkewe Hailey Bieber kwenye mtandao wa Instagram jambo ambalo limeibua mijadala mtandaoni.

Hatua hii inakuja kufuatia mfululizo wa matukio kama hayo ambapo Bieber amekuwa akifanya hivyo kwenye mitandao ya kijamii, ikiwa ni pamoja na kuacha kufuatilia watu wake muhimu akiwemo menta wake kwenye muziki Usher Raymond, meneja Scooter Braun, na hata kum-block baba mkwe wake Stephen Baldwin.

Hadi sasa, hakuna taarifa rasmi kutoka kwa wanandoa hao kuhusu sababu ya kufanya hivyo. Kwa upande wa mashabiki wametoa mitazamo yao wakidai huenda Bieber anapitia changamoto katika mahusiano yake.

Bieber na Hailey walianza urafiki wakiwa wadogo mwaka 2009 na kuingia rasmi kwenye mahusiano 2018 na Agosti 2024 walibarikiwa mtoto wao wa kwanza wa kiume Jack blues Bieber.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags