Chumba kilichoki kimya zaidi duniani cha Microsoft kilichopo jijini Redmond kimeingia katika Kitabu cha Rekodi za Dunia cha Guinness, kama sehemu tulivu zaidi duniani.Kikipiku chumba kilichopo Orfield Labs huko Minneapolis.
Ukimya wa chumba hicho huzifanya sauti ndogo mfano za mapigo ya moyo kusikika kwa ukubwa na kupelekea wageni wengi wanaotembelea chumba hicho wakishindwa kukaa kwa muda mrefu.
Chumba hiki ambacho awali kilijengwa kwa ajili ya majaribio ya bidhaa za kampuni za Microsoft, kama vile microphones, Spika huzuia kelele zote za nje ili kuwasaidia wahandisi waweze kurekebisha vifaa vya kielektroniki kwa usahihi.
Unaambiwa hata ndege ikipita karibu ya eneo hilo mtu aliyemo ndani atasikia sauti ya chini sana kama amenong’onezwa na mtu aliyekaribu naye.
Aidha baada ya eneo hilo kuwavutia wengi, kampuni hiyo ilianza kutoza fedha kwa watu watakaohitaji kuingia katika chumba hicho. Gharama zake ni dola 200 hadi 400 kwa mtu mmoja na dola 600 kwa saa moja.
Leave a Reply