Mwanamitandao na mwigizaji nchini Best King ambaye kwa sasa ni baba wa mtoto mmoja wa kike anayeitwa Chloe, ameweka wazi matamanio yake kwa binti yake kuhusu kazi atakayoifanya miaka ijayo.
Akizungumza na Mwananchiscoop amesema anatamani binti yake awe huru kufanya chochote ilimradi asivunje sheria za Mungu na maadili ya Mtanzania.
"Mimi natamani awe huru kuchagua kile anachokipenda, nitafurahi achague njia yake nzuri ambayo inampendeza Mungu na haivunji sheria. Ila iwe nzuri mimi nitakuwa tayari kumsapoti mimi nitakuwa tayari kufuata kile anachokipenda," amesema Best King
Amesema mara nyingi challenge zake kutofanya na mama wa mtoto wake ni kwa sababu hupendelea kukaa nyuma ya kamera na badala yake hufanya na shemeji anayefahamika kama Maria Kairanga.
"Mama Chloe anapenda kukaa nyuma ya kamera na kazi anayoifanya ni mtu wa filamu na anapenda kukaa nyuma ya kamera kwa sababu yupo kwenye timu ya Juakali kwahiyo kukaa mbele ya kamera labda mimi nimlazamishe," amesema .
Amesema anapendelea kufanya challenge za muziki kwa sababu ni shabiki mkubwa wa tasnia hiyo na muziki ni maisha yake.
"Mimi ni shabiki mkubwa wa muziki na wasanii wengi nawashabikia. Muziki ni maisha yangu kwa hiyo mara nyingi tunaongea kuangalia muziki wetu wa Bongo Fleva uweze kufika mbali tunashikana mikono kama vijana kama Watanzania tunaotamani kufika mbali," amesema
Amesema tofauti na kutengeneza maudhui ya mtandaoni na kuigiza pia anatamani kuwa mwandaaji wa filamu na kuanzia biashara ya mavazi na mitindo.
"Nipo na vitu tayari nimeshavifanya ila natengenezea mikakati mizuri kwa watu nikiwasilisha viwe vizuri. Nipo kwenye uzalishaji wa mwisho wa baadhi ya filamu nitakazoweka kwenye akaunti yangu ya YouTube kuanzia Septemba 2025.
“Kwenye mafanikio yoyote lazima maumivu yawepo ila mimi ni mtu ambaye sijali sana. Naweza nikawa napitia wakati mgumu sana lakini huwezi nikuta naonesha ugumu naopitia.
“Mimi nimepitia wakati mgumu sana kwa ambao nimekuwa nao wananijua wanaweza kuwa mashahidi. Lakini sijawahi kuwa muumini wa kuanza kuyafikiria matatizo,”amesema

Leave a Reply