Bien Amkingia Kifua Marioo Kuhusu Show

Bien Amkingia Kifua Marioo Kuhusu Show

Mwanamuziki kutoka Kenya ambaye ameshinda tuzo ya Trace Award katika kipengele cha msanii bora Afrika Mashariki, Bien amemkingia kifua Marioo baada ya wadau na muziki kumnanga kuhusiana na performance yake katika tuzo hizo.

Wakati alipowasili Kenya akitokea Tanzania ambapo tuzo hizo zilikuwa zikitolewa kwa mara ya kwanza alizungumza na waandishi wa habari huku akiwataka watu kuacha kumsema Marioo kwani ni msanii bora zaidi Bongo.

“Jamani tusiwe tunawabomoa watu nadhani Marioo ndiye msanii wa Bongo anayefuatiliwa zaidi nchini Kenya kwa sasa, Marioo ni mchapakazi, ni mtu mzuri vyovyote watakavyoongea kuhusu perfonance haijalishi mimi najua Marioo ni msanii bora.

Amenijenga amenirudisha mjini Marioo ni Brother wangu, hata sasa hivi nikiangalia Tiktok yangu naona watu wanavyofuatilia na kufanya challenge inaonesha nimepata mashabiki wapya,”amesema Bien

Kwa siku kadhaa sasa Marioo amekuwa akipokea maoni tofauti tofauti kutoka kwa mashabiki na wadau kuhusiana na performance yake aliyoifanya katika jukwaa la ugawaji wa tuzo za Trace zilizofanyika Visiwani Zanzibar huku wakidai kuwa msanii huyo hawezi kufanya live performance.

Marioo na Bien wanawimbo wa pamoja uitwao ‘Nairobi’ kutoka katika album ya Bad ‘The God Son’ ambapo mpaka kufikia sasa umetazamwa zaidi ya mara milioni 10 kupitia mtandao wa YouTube.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags