Elon Musk Ni Baba Wa Watoto 14 Sasa

Elon Musk Ni Baba Wa Watoto 14 Sasa

Tajiri na mmiliki wa mtandao wa X (zamani Twitter) Elon Musk ameongeza familia mbapo kwa sasa ameripotiwa kupata mtoto mwingine wa 14.

Taarifa hiyo imetolewa na mpenzi wake Shivon Zillis mwenye umri wa miaka 39 kupitia mtandao wake wa X ambapo alithibitisha kujifungua mtoto wa 14 wa bilionea huyo huku mpaka kufikia sasa wawili hao wakiwa na watoto wanne waliowapata pamoja.

Utakumbuka kuwa wiki chache zilizopita mpenzi mwingine wa Musk, Ashley St Clair (26) alitangaza kupata mtoto wa 13 na tajiri huyo huku akiweka wazi sababu ya kutotangaza muda wote na kudai kuwa ni kumlinda mtoto wake.

Aidha wiki iliyokwisha tajiri huyo aliingia katika vichwa vya habari vingi baada ya mzazi mwenzie Grimes akilalamika Musk kutopokea simu wakati mtoto wake anaumwa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags