Burna Boy awaunganisha Sautsol Kenya

Burna Boy awaunganisha Sautsol Kenya

Usiku wa kuamkia leo supastaa wa Nigeria, Burna Boy amefanya onyesho la muziki ambalo limeacha historia katika mji wa Nairobi nchini Kenya.
Tamasha hilo ambalo lilitawaliwa na amani likionesha umahiri wa Burna kwa kutoa burudani ambayo mashabiki wengi wameisifia kuwa miongoni mwa 'paformance' kali kuwahi kutokea nchini humo.

Kivutio kikubwa katika onyesho hilo ni baada ya wasanii waliokuwa wakiunda kundi la Sauti Sol Kenya, kuingia kwa kushtukiza nakuungana na Burna Boy jukwaani na kutumbuiza wimbo wa 'Time Flies' waliyoshirikishwa na msanii huyo kutoka kwenye albamu yake ya Twice As Tall iliyotoka Agosti, 13, 2020.

Hii inakuwa mara ya kwanza kwa Burna Boy kutumbuiza Live wimbo huo na Sautsol tangu kuachiwa kwake miaka mitano iliyopita na kupelekea mashabiki kusifu kuwa ni wakati wa kihistoria kwa muziki wa Kenya.

Tiketi za viingilio kwa VVIP katika tamasha hilo ziliuzwa kwa sh 65,000 za Kenya na ukumbi ulijaa sana, lakini pia inaripotiwa kuwa Burna Boy amelipwa dola milioni 1sawa na zaidi ya bilioni 3, huku akisafiri na timu ya watu 61 ambao ni pamoja na madansa, watu wa mitindo, ulinzi na watu wa bendi yote hiyo ili kuhakikisha tamasha hilo linakuwa nilakuvutia.
Kwa ufupi, tamasha la Burna Boy lililofanyika Uhuru Garden katika mji wa Nairobi, Kenya lilikuwa la aina yake na lakukumbukwa.

Hata hivyo, Msanii Harmonize alikuwa mmoja wa walio hudhuria shoo hiyo na alitakiwa kutumbuiza pamoja na Burna Boy lakini kutokana na kutofika kwenye maandalizi ya pafomance hiyo hakurusiwa kupanda jukwaani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags