Kufuatia changamoto ya kimazingira ambayo ilipelekea baadhi ya Tuzo za Trace Music Awards kushindwa kukabidhiwa kwa wahusika siku ya ugawaji wa tuzo hizo visiwani Zanzibar Februari, 26, 2025. Trace wameandaa usiku maalum kwa ajili ya kuwakabidhi badhi ya washindi wa tuzo hapa Tanzania.
Msanii Nandy ambaye alishinda tuzo katika kipengele cha Msanii Bora wa Kike nchini Tanzania, ameipokea tuzo yake usiku wa kuamkia leo kwenye hafla hiyo fupi iliyofanyika Johari Rotana Hotel Dar es Salaam.
Pia, Juma Jux ambaye alishinda tuzo ya Msanii Bora wa Kiume nchini Tanzania ameipokea tuzo hiyo usiku wa leo.
Jux na Nandy ambao ni washindi wa Trace Music Award baada ya kupokea tuzo hizo usiku wa kuamkia leo wameongelea furaha yao.
“‘Hii si kwa ajili yetu. Ni kwa ajili ya Tanzania, ni kwa ajili ya utamaduni, kwahiyo pongezi kwa mashabiki zetu na wote wanaotusapoti,’ amesema Nandy.

Leave a Reply