Mwigizaji wa Marekani ambaye alipata umaarufu kupitia filamu ya ‘Home Alone’ Macaulay Culkin amefunguka kuwa alimwaga machozi baada ya mdogo wake Kieran Culkin kushinda Tuzo za Academy ‘Oscar’ za 2025.
Wakati alipokuwa kwenye mahojiano na ‘Entertainment Weekly’ jana Jumatano Machi 4, 2025 alieleza kuwa wakati wa utoaji wa tuzo hizo aliangalia kipengele kimoja tu cha Best Supporting Actor ambacho mdogo wake ameshinda tuzo hiyo.
“Ni Best Supporting Actor tu. Hicho ndicho pekee nilichotazama, hii ilikuwa hadithi ya kweli, nililia sana na nikasema. Nitakuona baadaye,” amesema Culkin
Kieran Culkin alishinda Oscar katika kipengele cha Best Supporting Actor kupitia filamu ya ‘A Real Pain’ huku akiwapiga chini waigizaji kama Yura Borisov (Anora), Edward Norton (A Complete Unknown) na Guy Pearce (The Brutalist).
Macaulay na Kieran Culkin wote walianza kuigiza tangu walivyokuwa watoto huku wakionekana katika filamu kama Home Alone na nyinginezo.

Leave a Reply