Yaliyofanyika Kusafisha Jina La Burna Boy Kuhusu  Diddy

Yaliyofanyika Kusafisha Jina La Burna Boy Kuhusu Diddy

Baada ya mkali wa Hip-Hop kutoka Marekani Sean Combs ‘Diddy’ kukamatwa Septemba 16, 2024 na kutupwa katika gereza la Metropolitan, majina ya baadhi ya mastaa yalichafuliwa na kutajwa kwa namna fulani katika kesi zinazomkabili huku mmoja wapo akiwa ni mkali wa Afrobeat, Burna Boy.

Burna alikutana na Diddy kwa mara ya kwanza mwaka 2021 ambapo, Combs alimsaidia Burna kutengeneza album yake liyoshinda tuzo ya Grammy, ‘Twice as Tall’, kwa njia ya Zoom, ambapo kufuatia na matukio hayo mashabiki wamekuwa wakimuhusisha mkali huyo wa Afrobeat na masuala ya unyanyasaji wa kingono.

Kutokana na sakata hilo lililopelekea msanii huyo kupoteza baadhi ya madili yanayogharimu Sh 3 Bilioni na kupokea maoni mabaya katika mitandao ya kijamii. Timu yake ya PR ilifanya haya kusafisha jina katika kesi za Diddy.

Kwanza, mahusiano yake ya uongo na Chloe Biely, wawili hao walishika vichwa vya habari kwa wiki kadhaa zilizopita huku ikidaiwa kuwa mwanadada Biely alilipwa kusafiri mpaka jijini Lagos kuigiza kama mpenzi wa Burna. Na baada ya kurudi Marekani wawili hao walitemana ambapo msichana huyo alifuta urafiki kabisa na African Giant huyo kupitia mtandao wa Instagram.

Pili ishu ya kumuahidi mrembo mmoja gari aina ya ‘Lamborghini’, drama hizo zinaelezwa kuwa haziwezekani, kwani Burna hawezi kumpatia binti ndinga bure wakati anaweza kupata pisi kali bila ya kutumia gharama kubwa. Ambapo inadaiwa kuwa huwenda wanadada huyo amelipwa kwa ajili ya tukio hilo.

Mbali na matukio hayo ambayo yanafanywa na PR kwa ajili ya kusafisha jina la Burna kwenye kesi za Diddy, lakini pia yapo madai mengine ambayo yalieleza kuwa wiki chache zilizopita kuna moja ya mwanamke alifichua kwamba anaujauzito wa msanii huyo na kwamba amekataa kulea mimba.

Ishu ya msanii huyo kuhusishwa katika kesi za kingono haikuwa ndogo kwani kwa sheria za Marekani jina la Burna lingeendelea kutajwa asingeweza kuruhusiwa kutumbuiza nchini humo. Lakini baada ya kulisafisha kwa kufanya drama mbalimbali msanii huyo sasa anaweza kupiga show popote.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags