Diddy Apindua Meza, Ataka Kuachiwa Huru

Diddy Apindua Meza, Ataka Kuachiwa Huru

Mwanamuziki na mfanyabiashara maarufu Sean “Diddy” Combs ameamua kupindua meza, hii ni baada ya kutaka afutiwe makosa mawili yaliyobaki kwa kudai kuwa hakuvunja sheria yoyote kupitia makosa hayo.

Kulingana na nyaraka mpya zilizowasilishwa mahakamani usiku wa Jumatano, Julai 30,2025 na mawakili wa Diddy, wanataka Jaji Arun Subramanian kubadilisha hukumu hiyo kwani rapa huyo hana hatia ya makosa ambayo anatarajiwa kutolewa hukumu mwezi Oktoba.

Katika hoja zao, mawakili wa Diddy wanasema mteja wao hajawahi kufanya malipo kwa ajili ya ukahaba, hajawahi kushiriki tendo la ndoa na kahaba yeyote, wala kupanga kusafirisha watu hao, hivyo basi jambo hilo linamfanya rapa huyo kutokuvunja sheria ya Mann.

Aidha ushahidi uliotolewa mahakamani mwezi uliyokwisha pia haukuonyesha kuwa Diddy alijihusisha kimwili na watu hao, bali alihusishwa tu na kurekodi au kutazama matukio ya kingono yaliyofanywa na watu wazima kwa hiari yao.

Mawakili hao walidai kuwa wanawake waliokuwa wakihusika na matukio hayo ndio ambao walihusika kupanga kila kitu kuanzia usafiri, malipo pamoja na malazi ya watu hao.

Hata hivyo katika nyaraka hizo mawakili walidai kuwa wanaume ambao walihusishwa katika matukio hayo walikubali kwa hiari yao lakini pia walikuwa ni marafiki wa karibu wa Cassie Ventura na Jane.

Katika hoja nyingine, Diddy anadai kuwa matukio hayo yalikuwa yanalindwa kwani yalikuwa yakihusishwa na utayarishaji wa filamu za ngono ambazo zisizo za kibiashara zilizoandaliwa kwa matumizi ya baadaye.

Endapo mahakama haitafuta hukumu hiyo inayotarajiwa kutolewa Oktoba 3,2025, mawakili wa Diddy watafungua kesi mpya, ambapo ushahidi utakaoletwa utahusiana tu na mashtaka ya Sheria ya Mann huku wakiomba video ya kumpiga Cassie isihusishwe katika kesi hiyo ya RICO kwani tayari rapa huyo alikutwa hana hatia na kufutiwa mashtaka hayo.

Kwa sasa, Diddy yupo katika gereza la MDC Brooklyn. Gereza pekee la shirikisho jijini New York, ambapo mastaa wengine waliowahi kuwepo akiwemo mwimbaji R Kelly, Ghislaine Maxwell na mfanyabiashara wa sarafu ya kidijitali Sam Bankman-Fried nk






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags