Fahamu Faida Ya Kutumia Toner Usoni

Fahamu Faida Ya Kutumia Toner Usoni

Na Glorian Sulle

Ushawahi kujiuliza ni ipi faida ya toner kwenye ngozi? Basi leo acha tukufahamishe ni ipi kazi ya toner na faida nyingine katika kutunza ngozi. 

Ili kufanikisha wewe msomaji wetu kufahamu zaidi kuhusu hili, Mwananchi Scoope imezungumza na mtaalamu wa ngozi, Ritha Peter ambapo anasema: “Toner ni bidhaa ya urembo inayotumika kwenye ngozi baada ya kusafisha uso na kabla ya matumizi ya moisturizers au serums, bidhaa hii hurudisha PH ya ngozi kwenye kile kiwango cha kawaida baada ya kusafisha na kuondoa uchafu wa mabaki ya sabuni au make up." 

Ritha anasema kazi kubwa ya bidhaa hiyo ni kutengeneza unyevu kwenye ngozi, na kuwa bidhaa hiyo inaweza kuwa na viambatano kadha wa kadha kulingana na aina ya ngozi.

“Kuna toner ya ngozi ya mafuta, mara nyingi aina hii ya kipako ina viambato vya kupunguza mafuta kama kwenye ngozi kama vile witch hazel au salicylic acid,” anaeleza. 

Anasema pia, kuna toner ya ngozi kavu ambayo lazima iwe na viambato vya kuongeza unyevu kama vile aloevera, hyaluronic acid, au glycerin.

“Kiambato kingine cha ngozi nyeti (dilicate skin) inakuwa na viambato vya utulivu kama vile   chamomile au rose water, ili kupunguza uchochezi na kulinda ngozi za aina hii,” anaeleza.

 

FAIDA ZA TONER

 Ritha anasema faida ya kipako hiki katika ngozi hupunguza vipele na harara huku ikizuia upele kutokana na kuwa na viambata vinavyopambana na hali hiyo. 

“Ukiachana na ulinzi dhidi ya vipele bidhaa hii pia hupunguza maumivu ya mionzi ya jua na kuitengeneza tena ngozi iliyochomwa na jua kwa kuipatia unyevu na kupunguza maumivu kwenye mashavu na sehemu zinginezo,” anaeleeza.

Kadhalika anasema inarudisha kwenye ubora wake kwa kuipa unyevu na kuchochea mzunguko wa ndani.

“Inapunguza madoa na mabaka, huondoa makunyazi katika ngozi na kisha inapambana na bakteria waliopo kwenye ngozi na mwisho huboresha hali ya ngozi kwa kuzuia kuzeeka mapema kwa kuchochea collagen na elastin,” anaeleza.

 Pia Ritha anasema toner ni kati ya hatua muhimu katika utunzaji wa ngozi inayosaidia kurejesha nuru ya ngozi, kutoa unyevu na kuifanya ngozi kuwa tayari kupokea bidhaa za urembo.

“Kuna wakati tunaharibika ngozi na hatufahamu sababu, mara nyingi wengi hununua bidhaa nzuri za urembo ila hawafahamu matumizi sahihi huhitaji usahihi wa matumizi ya bidhaa walizonazo kwa kufuata ushauri wa wataalamu wa ngozi ili kupata matokeo sahihi na waliyo yategemea,” anaeleza.

 Kwa andiko hili, nina imani na hakika msomaji wetu utakuwa umejua namna sahihi ya kutumia vipako vyetu ili kupata matokeo sahihi ya bidhaa zako za urembo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags