Jina La Utani Lilivyomkimbiza Madonna Uingereza

Jina La Utani Lilivyomkimbiza Madonna Uingereza


‘Material Girl’ ni wimbo wa mwanamuziki kutoka Uingereza Madonna ambao aliuachia rasmi Januari 23, 1985 wimbo huo ulimpatia mafanikio makubwa ya kimuziki pamoja na kusaini mikataba mbalimbali ya kibiashara kutokana na wimbo huo kupendwa zaidi.

Mbali na kuwa mkubwa pia ulikuwa katika album ya msanii huyo iitwayo ‘Like a Virgin’ ulimpatia jina la utani akiitwa ‘Madge’ kutokana na maudhui ya wimbo ambayo yanahusiana na maisha ya kifahari.

Madonna hakupendezwa na jina hilo kitendo ambacho kilimfanya kuondoka Uingereza na kurudi Marekani huku akifunguka kuwa jina hilo lilimfanya ahisi wa kawaidi sana.

Ngoma ya ‘Material Girl’ imewahi kupanda hadi nafasi ya pili kwenye chati za muziki Marekani huku ikiingia kwenye tano bora katika baadhi ya maeneo kama Uingereza, Australia, Ubelgiji, Canada, Ireland, na Japan.

Madge jina hili linatokana na neno la Kiingereza Maegen, ambalo lina maana ya "msichana mchanga" au "bikira." Linaweza pia kumaanisha "lulu" au "maridadi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags