Rapa kutoka Marekani ameeleza kuwa mwanamuziki Chris Brown kama asingemfanyia vurugu na kuwafanya mashabiki wamchukie kwa kitendo chake basi angekuwa katika kiwango ambacho alikuwa nacho marehemu mfalme wa Pop, Michael Jackson ‘MJ’.
Wakati alipokuwa kwenye moja ya mahojiano yake ameeleza kuwa tukio ambalo Breezy alilifanya akiwa na miaka 19 limeathiri sana heshima na mafanikio yake ya kitaaluma.
“Kama si tukio lile na Rihanna, Chris Brown angekuwa karibu kabisa na tulichowahi kuona kama Michael Jackson. Kwa upande wa kipaji, yeye ndiye msanii wa kushangaza zaidi wa wakati wetu.
Jamaa anaweza kuimba, kucheza, kuchora... ni kipaji cha pande tatu. Lakini kosa lile alilofanya akiwa na miaka 19 limeathiri sana heshima na mafanikio yake ya kitaaluma,”amisema Fat
Mara kadhaa Breezy katika mahojiano yake amekuwa akieleza kuwa anamtazama MJ kama role model wake na kwamba alijifunza mengi kutoka katika kazi za msanii huyo, jambo ambalo linamfanya aendelee kufanya kazi kwa bidii kufikia levo zake.
Utakumbuka kuwa Februari 2009, usiku wa tukio la ugawaji wa tuzo za Grammy Awards, Chris Brown alimpiga Rihanna kwa nguvu, kumng’ata, na kusababisha majeraha makubwa usoni na mwilini jambo ambalo lilimfanya Breezy kukamatwa na polisi.
Aidha baada ya ugomvi huo wawili hao walipatanishwa tena na mwaka 2012 walitoa ngoma ya pamoja iitwayo ‘Nobody’s Business’ wimbo ambao walichukua baadhi ya mashairi katika wimbo wa Michael Jackson "The Way You Make Me Feel.".

Leave a Reply