Hii Ndio Maana Ya RN3 Ya Mbosso

Hii Ndio Maana Ya RN3 Ya Mbosso

Baada ya kuwepo kwa tetesi katika mitandao ya kijamii kuwa mwanamuziki Mbosso naye anatarajia kuoa kufuatia na hastag ya ‘RN3’ aliyoiweka katika Instagram yake. Hatimaye msanii huyo ameweka maana ya neno hilo akiwa na maana ya ujio wake mpya.

Kwa takribani miezi mitano msanii huyo alikuwa kimya baada ya kutoka katika lebo ya WCB mapema mwaka huu huku taarifa hizi zikithibitishwa na aliyekuwa bosi wake Diamond ambapo aliondoka katika lebo hiyo kwa makakubaliano ya baina ya wote wawili bila hata kutoa kiasi chochote cha fedha.

Ikumbukwe Mbosso alijiunga na lebo hiyo mwaka (2018) akiwa ni msanii wa sita kusainiwa na WCB Wasafi baada ya Harmonize (2015), Rayvanny (2016), Queen Darleen (2016), Rich Mavoko (2016), Lava Lava (2017), Zuchu (2020) na D Voice (2023).

Mbosso anaenda kuongezeka katika orodha ya wasanii waliojitoa kwenye lebo hiyo. Hadi sasa wamekuwa wa nne, alianza Rich Mavoko (2018) akaanzisha lebo yake Billionea Kid, Harmonize (2019) akaanzisha Konde Music Worldwide na Rayvanny (2022) akaanzisha Next Level Music (NLM).






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags