Mama Carina Afariki Dunia, Apishana Siku 40 Na Mwanaye

Mama Carina Afariki Dunia, Apishana Siku 40 Na Mwanaye

Fatma Maruzuku ambaye ni mama mzazi wa Marehemu Hawa Hussen (Carina), amefariki dunia leo June 06,2025 jijini Dar es Salaam.

Kaka wa Marehemu amethibitisha kutokea kwa msiba huo, ambapo amesema dada yake alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya Presha na Kisukari.

Amesema kutokana na hali hiyo, marehemu hakuweza hata kushiriki Arobaini ya mtoto wake iliyofanyika wiki iliyopita.
Mama Carina atazikwa katika makaburi ya Kisutu kesho June 07,2025 saa 10 jioni.

Mwigizaji Hawa Hussein (Carina) alizikwa April 19, 2025 katika Makaburi ya kisutu Dar es Salaam baada ya kufariki India alipokuwa akipatiwa matibabu kutokana na matatizo ya tumbo yaliyokuwa yana msumbua.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags